Sunday, November 23, 2014

shambulio lla basi kenya lina madhara gani ki din na kisiasa

watu wanaoaminika ni wafuasi wa Al-shabab wamewaua watu wapatao 28 kwenye shambulio la basi lililokuwa linaelekea kwenye mji mkuu wa Kenya,Nairobi,tukio hilo limetokea mpakani kabisa mwa Somalia.Kikundi cha kiislamu cha Al-Shabab kimeanza mashambulizi dhidi ya Kenya Tangu 2011,na BBC iilifanikiwa kumuhoji mtu anaeaminika alikuwa anashuhudia tukio amesema baada ya kufanikiwa kusimamisha basi hilo huku wakiongea Kisomali waliwapiga risasi abiria wote ambao sio Wasomali,shahidi huyo alisema
Basi hilo lililokuwa limebeba abiria 60 lilitekwa nyara alfajiri na abiria 28 walipigwa risasi na kuuwawa.
Wengi waliouwawa ni kutoka maeneo mengine ya Kenya ambao wakifanya kazi Mandera.
Inasemekana kuwa wengi wao walikuwa waalimu na wafanyakazi wa wizara ya afya ambao walikuwa wanarudi nyumbani kuwa na familia zao wakati wa Noeli.
Msemaji wa wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, alidai kuwa walihusika na shambulio hilo.
Wanajeshi na polisi wametumwa huko kwenda kuwasaka wale waliohusika na shambulio hilo lakini hakuna taarifa kuwa wamekamatwa.

0 comments:

Post a Comment