Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi.

Sijui imekuwaje nawaza sikustahili hali hii lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza.

Mwenye sifa zifuatazo:

  1. Muislamu au awe tayari kuwa muislamu.
  2. Asiwe mtoto, na asiwe anakaribia miaka 40.
  3. Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa.
  4. Awe tayari kuolewa (akinipenda) na kupata watoto.
  5. Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.


Baadhi ya wasifu wangu:

  1. Sina mtoto na sijawahi kuoa.
  2. Ninakazi na elimu ni shahada.
  3. Ninajitegemea katika maisha ya kawaida, ni msaada kwa baadhi ya ndugu zangu na, ni mchapa kazi na mpenda maendeleo.
  4. Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
  5. Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (5’5”), rangi ni nyeusi kiasi.